Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Mei, 2018

China yapinga shutuma za Marekani kuhusu uhamisho wa teknolojia

Balozi wa China katika Shirika la biashara duniani WTO Bw. Zhang Xiangchen amepinga shutuma za Marekani kuwa China imetumia vibaya makubaliano ya mahitaji ya ubia na kuchukua teknolojia, akisema Marekani ni nchi inayonufaika zaidi kutokana na uhamishaji wa teknolojia. Akiongea kwenye mkutano wa WTO kuhusu utatuzi wa migogoro DSB, Bw. Zhang ameeleza kuwa teknolojia zinazohamishwa kutoka kampuni za Marekani kwa kampuni za China ni shughuli za kawaida zinazofanyika kwa mujibu wa makubaliano yaliyofikiwa kati ya pande mbili, pamoja na matakwa ya kampuni, hatua ambayo inafuata kanuni za biashara huria na ushindani kwenye soko. Pia amesisitiza kuwa ukaguzi wa kipengele cha 301 cha sheria ya biashara ya Marekani hauwezi kutoa ushahidi kuthibitisha kuwa sheria za China zinayalazimisha makampuni ya kigeni kutoa teknolojia kwa washirika wake wa China, wala haukutoa ushahidi kwamba China imekiuka kanuni za WTO kwa kuweka utoaji wa teknolojia kama sharti kwa uwekezaji wa kigeni kuingia nchini...

Siku ya Walinda Amani Duniani-Juhudi za Jeshi la Kenya kulinda amani nchini Somalia

Picha
Siku ya Walinda Amani Duniani-Juhudi za Jeshi la Kenya kulinda amani nchini Somalia (GMT+08:00) 2018-05-29 08:45:21 Hii leo Kenya inaungana na nchi nyengine duniani kuadhimisha siku ya Walinda Amani Duniani.Kaulimbiu ya mwaka huu ya Siku ya Walinda Amani Duniani ni "Walinda Amani wa Umoja Mataifa:Miaka 70 ya Huduma na Kujitolea" Kenya inaadhimisha siku hii wakati ikiwa inafikisha miaka 7 sasa tangu wanajeshi wa Kenya kwenda kulinda amani nchini Somalia mwaka 2011. Mwandishi wetu Khamis Darwesh ametuandalia ripoti ifuatayo. Tarehe 29 Mei ni siku ambayo ilitengwa na Umoja wa Mataifa kusherehekea michango ya wanajeshi na raia katika shirika hilo na kuwapatia heshima walinda amani zaidi ya 3,700 ambao wamepoteza maisha yao wakihudumu chini ya mwamvuli wa Umoja Mataifa tangu mwaka 1948,ikiwa ni pamoja na 129 waliokufa mwaka uliopita. Jeshi la ulinzi la Kenya chini ya mwamvuli wa majeshi ya Umoja wa Afrika,AMISOM,limekuwa mstari wa mbele katika kuleta amani na kupa...

Ofisa Utumishi Mkuu Wa Mamlaka ya Mapato (TRA) Atoa Ushahidi Mahakamani Dhidi ya Mtumishi Wao Anayedaiwa Kumiliki Mali Nyingi

Picha
Ofisa Utumishi Mkuu Wa Mamlaka ya Mapato (TRA) Evans Emil ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa Ofisa Msaidizi wa Forodha wa TRA Jennifer Mushi anayedaiwa kumiliki magari 19 yasiyolingana na kipato chake anamiliki baadhi ya mali asilimia 50 kwa 50 na familia yake. Emil ambaye ni shahidi wa kwanza katika kesi hiyo ameyaeleza hayo wakati akijibu maswali ya wakili wa serikali Pius Hilla mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Wilbard Mashauri. Katika ushahidi huo Emil amedai kuwa July Mosi, 2011 Jennifer alipewa ajira na kupatiwa fomu mbalimbali ajaze ikiwamo fomu ya Tamko ya Rasilimali na madeni. Katika fomu hiyo ya rasilimali March 30,2012 imeonyesha Jennifer anamiliki fedha taslimu Sh.Laki 6 zilizopo katika benki na taasisi za fedha Sh 800,000. Pia alikuwa na Hisa na gawio la thamani ya Sh.Laki 6, anamiliki nyumba Kinyerezi Kichangani ya Sh.Mil 30 ambapo anamiliki asilimia 50 kwa 50 baina yake na mumewe, vilevile anamiliki shamba la Heka 1 Mabwepande lenye thamani ya Sh.Laki...

Kijana wa Mali aliyemuokoa mtoto ghorofani akutana na Rais, apewa uraia na kazi serikalini

Picha
Mhamiaji kutoka Mali amepewa sifa na kutunukiwa uraia wa Ufaransa baada ya kufanya tendo la kishujaa kwa kumuokoa mtoto mdogo aliyekuwa ananing’inia kwenye kibaraza cha ghorofa ya nne katika jengo refu jijini Paris. Mamoudou Gassama, mwenye umri wa miaka 22 alipanda jengo hilo refu bila kutumia vifaa vyovyote huku akishangiliwa na watu waliokuwa wamekusanyika nje ya jengo hilo, hadi kufanikisha kumfikia mtoto huyo wa kiume mwenye umri wa miaka minne. Kitendo hicho cha kishujaa kilichofananishwa na ushujaa uliwahi kuoneshwa na ‘Spiderman’, uliteka mitandao ya kijamii huku video yake ikivuta hisia za wengi waliotaka atunukiwe uraia na maisha bora kwa kujitoa kuokoa maisha. Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron alimualika kijana huyo Ikulu na kuzungumza naye, kisha akampa cheti maalum cha kutambua ushujaa wake na kuamuru apewe uraia wa Ufaransa baada ya kusikia jinsi alivyohangaika kuingia nchini humo. Lakini pia Rais Macron amempatia kazi Mamoudou katika jeshi la zima moto la ...

Breaking News: Kinana ang'atuka nafasi ya Ukatibu Mkuu CCM ....Tazama Hapa Majina ya Waliochaguliwa NEC Ya CCM

Picha
Katibu mkuu Taifa wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana ameng'atuka nafasi yake aliyokuwa akiishika ndani ya chama hicho na CCM wameridhia ombi hilo rasmi. Hayo yamewekwa wazi na taarifa zilizotolewa na Katibu wa NEC-Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole leo Mei 29, 2018 na kusema kwa pamoja wamemtakia mafanikio mema katika shughuli zake. "Napenda kumshukuru ndugu Kinana kwa utumishi wake katika Chama cha Mapinduzi (CCM) na CCM itaendeleaq kutumia uzoefu wake katika majukumu mbalimbali ya chama kwa kadiri itakavyohitajika", imesema taarifa hiyo. Kwa upande mwingine, Kinana wakati anatoa neno lake la kuwaaga wajumbe wa NEC amewasisitizia wajumbe hao na wana CCM kiujumla kudumisha umoja wa wanachama na chama cha mapinduzi (CCM).

Kagera: Mke Amuua Mume Wake Kisa Wivu wa Mapenzi

Picha
Victoria Salvatory (58), mkazi wa kata ya Katoma, Kagera anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumuua mumewe, Salvatory Iteganira (62) kwa kile kinachodaiwa ni wivu wa kimapenzi. Kamanda wa Polisi mkoa wa Kagera, Augustino Ollomi amesema mauaji hayo yalitokea jana saa 6:00 mchana. Akizungumza leo Mei 28, Kamanda Ollomi amesema mtuhumiwa anadaiwa kumpiga mumewe kwa kitu kizito kichwani na kumsababishia jeraha lililovuja damu nyingi na hatimaye kifo. “Wanandoa hao wanadaiwa kuwa na ugomvi ambao chanzo chake tunaendelea kuchunguza; baada ya ugomvi huo mtuhumiwa alimpiga mume wake kichwani kwa kitu kizito kilichosababisha jeraha lililovuja damu nyingi na kusababisha kifo chake,” amesema Ollomi. Kamanda huyo amewaasa wanandoa na wapenzi kutumia njia ya majadiliano, usuluhishi na sheria kutatua tofauti miongoni mwao badala ya kujichukulia sheria mikononi.

BREAKING: Rais Magufuli Afunguka KINANA Kujiuzulu

Picha

RAYVANNY FT.khaligraph/Godzilla/rosa ree/izzo bizness/countryboy/young d...

Picha

RAYVANNY FT.khaligraph/Godzilla/rosa ree/izzo bizness/countryboy/young d...

Picha

Matangazo ya vyakula mitandaoni huponza watoto

Picha
Mitandao ya kijamii huenda ikachochea watoto kula vyakula visivyofaa, utafiti umeeleza Umegundua kuwa watoto wanaojihusisha sana na kutazama mitandao hii wakiona watu wanatumia vyakula vyenye sukari na mafuta kwa wingi nao huiga kwa kula vyakula vyenye asilimia 26% ya vyakula hivyo zaidi kuliko watoto wasiofuatilia mitandao. Utafiti, uliowasilishwa kwenye Bunge la Ulaya kuhusu unene, ulichambua kuhusu muitikio wa watoto kutokana na picha za mitandaoni. Matokeo ya utafiti huoyamekuja baada ya kuwepo kwa wito wa kuweka sheria kali dhidi ya matangazo ya vyakula visivyo bora Nyota wa kwenye mitandao ya kijamii walioainishwa kwenye utafiti ni pamoja na Zoella, mwenye wafuasi milioni 10.9 kwenye mtandao wa Instagram na Alfie Deyes, mwenye wafuasi milioni 4.6. Watoto 176 waligawanywa kwenye makundi matatu na kuonyeshwa picha za watu maarufu wakitangaza kuhusu vyakula visivyo na afya, vyakula bora, na bidhaa zisizo chakula. walionyeshwa vyakula vilivyo bora na visivyo bora ili k...

Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 27.05.2018

Picha
Mlinda mlango wa Manchester City Joe Hart, 31, ameibuka kuwa chaguo la Manchester United kusaidia na David de Gea, 27. Baada ya meneja Jose Mourinho kuona mlinda mlango namba mbili Sergio Romero, 31 anataka kuondoka. (sun). Meneja wa zamani wa Arsenal Arsene Wenger, anatarajia kurejea Japan kuendelea na kazi yake ya ukocha.(Mail on Sunday). Juventus imezungumza na Atletico Madrid kuhusu uwezekano wa kumsajili mlinzi mwenye asili ya Uruguay, Diego Godin, 32.(Calciomercato) Wakati huo huo beki wa kulia wa Juve Stephan Lichtsteiner, 34, anajiandaa kujiunga na Arsenal bila malipo ya uhamisho.(London Evening Standard) Meneja Steve Bruce amemtaka kiungo wa kati Jack Grealish, 22, kubaki Aston Villa kwa msimu mwingine baada ya fainali ya michuano ya mabingwa.(Express and Star) Paris St-Germain mshambuliaji Neymar, 26,amerejea kauli yake kuwa ana shauku siku moja acheze chini ya meneja Pep Guardiola.(ESPN Brasil, in Portuguese) Everton inatarajia kutumia mwanya wa timu za Man...

Zidane:Najivunia kuwa sehemu ya Mafanikio ya Real Madrid

Picha
Zinedine Zidane amesema anajivunia kuweka historia na Real Madrid baada ya kunyakua taji la ligi ya mabingwa dhidi ya Liverpool siku ya Jumamosi. Real Madrid ilishinda mabao 3-1 huku Gareth Bale akifunga magoli mawili Real ni timu yenye mafanikio zaidi kwenye historia ya ligi ya mabingwa ikiwa na mataji 13. Zidane alisema:''hii ni klabu ya wakongwe. Klabu hii imeshinda makombe 13 ya Ulaya nafurahi kuwa sehemu ya historia hii Aliongeza: '' tunakwenda kufikiria kuhusu tulichokipata, kufurahia wakati huu kwanza.Ni kitu muhimu zaidi kwa sasa''. Timu tatu pekee zimeshinda kombe la mabingwa barani Ulaya, Real ikiwa na mataji matano tangu mwaka 1956, Ajax (1971-73) na Bayern Munich (1974-76). Hata hivyo Real ni ya kwanza tangu kubadilishwa kwa jina la michuano hiyo. Kiungo Luka Modric anaamini itakuwa ngumu kwa timu kufikia mafanikio ya Real ''Ni jambo la ajabu la kihistoria, aliiambia BT Sport ''Sijui kama kuna mtu atarudia hili...

Waziri Mkuu: Tujiepushe na Vitendo Vya Chuki

Picha
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka waumini wa dini ya Kiislamu wajiepushe na vitendo vinavyoweza kupandikiza chuki dhidi yao au kwa waumini wa dini nyingine. Ametoa kauli hiyo jana (Jumamosi, Mei 26, 2018) wakati akizungumza na viongozi na mamia ya waumini wa dini ya Kiislamu walioshiriki mashindano ya kitaifa ya kuhifadhi Quran tukufu kwenye ukumbi wa Mwl. J. K. Nyerere jijini Dar es Salaam. Mashindano hayo yaliyoandaliwa na Jumuiya ya Kiislamu ya Istiqaama Tanzania (Istiqaama Muslim Community of Tanzania), yalijumuisha washiriki 29 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara na Visiwani. “Serikali inatambua na inathamini sana, mchango wa dini katika kuwalea waumini kiimani na kutunza amani ya nchi. Hivyo, tujiepushe na kauli au vitendo ambavyo vinaweza kupandikiza chuki na uhasama dhidi yetu au dhidi ya waumini wa imani nyingine,” amesema. “Nitoe rai kwenu viongozi wangu na waumini wenzangu, tujenge misingi ya kuvumiliana na kustahamiliana. Hilo pekee ...

Makatibu Tawala wa Mikoa Waagizwa Takwimu za Wazee Ifikapo 30 Juni, 2018

Picha
Na. Atley Kuni-OR TAMISEMI Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa        Mhe. Selemani Jafo (Mb), amewaagiza Makatibu Tawala wa Mikoa Tanzania Bara kuwasilisha taarifa za takwimu za wazee ifikapo      30, Juni 2018. Waziri Jafo, alitoa kauli hiyo mapema jana alipokuwa akizindua  zoezi la kuwapatia vitambulisho maalum wazee wapatao 1,118 wa Jiji la Dodoma kutoka kata za Mkonze, Mnadani, Uhuru, Madukani, Makole na Majengo. Vitambulisho hivyo, pamoja na mambo mengine vitawawezesha wazee hao kupata huduma za afya bure na kwa wakati. “Ifikapo tarehe 15 Juni, 2018 kila kata iwe imetambua wazee na ifikapo tarehe 22 Juni, 2018 kila Halmashauri iwe imeunganisha taarifa za wazee kutoka katika kata zake zote” alisema Waziri. Aidha Waziri Jafo aliagiza kuwa, “ifikapo Juni, 26, 2018 kila Mkoa uwe umeunganisha taarifa zote na kuzituma kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI”. Aliwaonyawa...

Polisi Dar Wakusanya Milioni 972 Za Makosa Barabarani Ndani ya Wiki Mbili

Picha
Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limekusanya Sh972.7 milioni za makosa ya usalama barabarani katika kipindi cha wiki mbili. Katika operesheni hiyo ya ukamataji wa magari iliyofanyika kati ya Mei 11 hadi Mei 24, mwaka huu magari yaliyokamatwa ni 24,116, pikipiki 763 na daladala 10,301. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, kamanda wa kanda hiyo, Lazaro Mambosasa alisema, “Waendesha babodada waliofikishwa mahakamani kwa makosa ya kutovaa kofia ngumu na kupakia mishikaki (abiria zaidi ya mmoja) ni 59. Jumla ya makosa yaliyokamatwa ni 30,850 na fedha zilizopatikana ni Sh972 milioni. “Madereva na wamiliki wa magari wanatakiwa kulipa faini zao ndani ya siku saba ili kuepuka faini kuongezeka na kusababisha kukamatwa tena kwa kulimbikiza madeni,” alisema Mambosasa. Katika hatua nyingine; Mambosasa alisema polisi wanamshikilia mhudumu wa Hoteli ya Sleep Inn kwa tuhuma za kukutwa na sare za polisi, sil...