Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Agosti, 2016

Ukuta

Picha
Toka kwenye ukurasa wa Twitter account ya MillardAyo amepost hii picha na Maneno yaliyo Semwa na CHADEMA.

Simba Kumpeleka Kessy Mahakamani.

Simba imepanga kumpeleka Kessy mahakamani kwa madai ya kuwatuhumu viongozi wa Simba kuwa walitaka kumpa rushwa Klabu ya Simba imejiridhisha na kupeleka ushahidi kwenye kamati ya sheria na hadhi za wachezaji kuhusu sakata la usajili linalomhusu beki wa kulia wa Yanga Hassan Kessy Ramadhani na wanaamini endapo haki itasimamiwa vilivyo basi watashinda kesi hiyo. “Yanga walituandikia barua, TFF wakiomba kupewa leseni ya mchezaji Kessy kabla ya June 15 ambapo ndio ulikuwa mwisho wa mkataba wake, tena walikuwa wanamuombea leseni ya CAF lakini kimantiki huwezi kupewa laseni ya CAF bila kuwa na leseni ya ndani”, amesema Haji Manara afisa habari wa Simba wakati akizungumza na waandishi wa habari. “Kwahiyo kimsingi, Kessy alivunja mkataba, Yanga walimchezesha mchezaji ambaye aliwekewa pingamizi.” Wakati huohuo klabu ya Simba imepanga kumpeleka Kessy mahakamani kwa madai ya kuwatuhumu baadhi ya viongozi wa Simba kutaka kumpa rushwa wakati akiwa Mtibwa Sugar. “Ha...

Miamala ya Benk na Simu,Imezaa matunda.

Picha
31 AGOSTI 2016 Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango SHERIA ya Fedha ya Mwaka 2016 iliyopitishwa kuhusu utozaji ushuru kwenye ada ya kutuma na kupokea fedha kwenye miamala ya benki na simu, imeanza kuzaa matunda kutokana na ongezeko la mapato lililoanza kushuhudiwa kutoka kampuni za simu. Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu iliyokutana jana na Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA), iliambiwa kutokana na sheria hiyo iliyopitishwa Bunge baada ya kupitisha bajeti ya mwaka huu, mwezi uliopita serikali imeshuhudia ongezeko kubwa la mapato, yaliyotolewa na kampuni za simu. Taarifa hiyo ilitolewa jana kwenye Kamati ya Kudumu ya Miundombinu, imeonesha Kampuni ya Vodacom ilikuwa ikitoa kodi ya ushuru wa bidhaa kwa fedha zinazotumwa kwa wastani wa Sh milioni 360 kwa mwezi, lakini baada ya mabadiliko ya sheria, Julai pekee mwaka huu imelipa Sh bilioni 1.9. Mwakilishi wa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato (TRA), Godwin Barongo aliiambia kamati hiyo kuwa kwa upande wa Kampuni ya Tigo, wal...

Profesa Bensin Bana; UKUTA ni Ndoto ya mchana.

Picha
IMECHAPISHWA: 31 AGOSTI 2016 MSOMI maarufu nchini, Profesa Benson Bana na mwanasiasa aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi, Leticia Mosore wamesema maandamano yaliyopewa jina la Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania (Ukuta), hayawezekani kwani ni ndoto ya mchana na hayana msingi wowote wala tija kwa wahusika hata kwa Taifa. Aidha, maandamano hayo ya nchi nzima imeelezwa kuwa ndio kifo cha Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kwani kila chama kimekuwa kikihangaika kivyake. “Wanaotaka kuandamana wanajidanganya na kuwalaghai wenzao kwani kufanya operesheni ni suala la dola na si la mtu au kikundi cha watu, hivyo maandamano hayo hayawezekani kabisa,” alisema Profesa Bana katika mahojiano maalumu na Idara ya Habari (MAELEZO). Mhadhiri huyo Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, aliongeza kuwa wanaojiita Ukuta ni kwamba Rais John Magufuli amewanyima ajenda, kwani utendaji wake umezidi fahamu zao na kuwafanya waanze kutapatapa wasijue nini cha kufanya. Alise...

Tanapa Kuongeza Watalii Hifadhi ya Taifa ya Ruaha.

Picha
WETUIMECHAPISHWA: 31 AGOSTI 2016   Meneja Mawasiliano wa TANAPA,  Pascal Shelutete akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) wilayani Mbarali namna ambavyo TANAPA ilivyojipanga kwa ajili ya tukio la kupatwa kwa jua litalotarajiwa Septemba Mosi. Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Mbarali, Reuben Fune.(Mpigapicha Wetu) SHIRIKA la Hifadhi za Taifa (TANAPA) limetangaza kutumia tukio la kupatwa kwa jua linalotarajia Septemba mosi mwaka huu kufungua lango la Ikoga katika wilaya ya Mbarari mkoani Mbeya ili kuongeza watalii katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha.   Kufuguliwa kwa lango hilo kunafanya idadi ya milango ya kuingia katika hifadhi hiyo kufikia miwili ukiacha lango kuu la Way Junction ambalo limekuwa likitumika kwa muda mrefu sasa. Meneja Uhusiano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete  anasema kuongezeka kwa lango la Ikoga ni fursa kubwa ya kuhamasisha utalii wa ndani kwa kuwa eneo la Ihefu lina kivutio kikubwa cha wanyama wa aina mbalimbali. Mkuu wa...

Uturuki na Mashambulizi,YPG Kurudi nyuma,Wasi wasi wa Marekani.

Picha
Uturuki yaonya kuendelza mashambulizi Syria Uturuki imeonya kufanya mashamabulizi zaidi dhidi ya wanamgambo wa Kikurdi walioko Syria iwapo watashindwa kurudi nyuma huku Marekani ikilani mashambulio yao mwishoni mwa wiki kama jambo lisilokubalika. Uturuki imeendelea na operesheni zake kuu mbili ndani ya Syria dhidi ya wanajihadi wa kundi la Dola la Kiislamu na wapiganaji wa Kikurdi wa kundi la YPG kwa kushambulia kwa mizinga maeno yao kadhaa. Uturuki imesema imeuwa magaidi 25 wa Kikurdi katika maeneo yanayokaliwa na kikosi cha YPG nchini Syria ambacho Uturiki inakiona kuwa ni cha kigaidi hapo jana, siku moja baada ya mwanajeshi wa Uturuki kuuawa na shambulio la roketi lililorushwa na wanamgambo hao. Operesheni hiyo ya Uturuki inakusudia kuwarudisha nyuma wapiganaji wa kikosi hicho kupitia Mto Euphrates ili kuwazuwiya kuliunganisha eneo la mashariki mwa mto huo ambalo tayari liko kwenye udhibiti wao na lile lanaliloshikiliwa na Wakurdi lilioko magharibi. Kundi la YPG latakiwa kurud...

Kanseal Angela Merkel;Hajaamua juu ya kushiliki katika uchaguzi,Wakimbizi wabadilisha hali

Picha
Maoni : Kansela Angela Merkel hajaamua juu ya kushiriki katika uchaguzi Wakati wa uchaguzi wa mwaka 2013 mambo yalikuwa tofauti kwa Kansela Angela Merkel. Mapema kabla ya uchaguzi huo alitamka wazi kwamba hakuwa anawaza kuondoka kwenye wadhifa huo.Lakini kwa nini amenyamaza? Kansela wa Ujerumani Angela Merkel Kansela wa Ujerumani anawaweka Wajerumani katika hali ya tashwishi.Hawajui iwapo Kansela huyo atawania muhula mwingine.Hata hivyo mnamo mwaka wa 2011 mambo yalikuwa shwari kabisa nchini Ujerumani. Migogoro ya wakati huo ilikuwa mbali na Ujerumani. Ilikuwapo katika nchi nyingine za Umoja wa Ulaya. Umaarufu wa Kansela Merkel miongoni mwa wananchi ulikuwa wa kiwango cha juu kabisa .Kampeni za uchaguzi zilikuwa za upande mmoja na hasa juu yake. Mgogoro wa wakimbizi wabadilisha hali Lakini mgogoro wa wakimbizi tangu mwaka uliopita umebadilisha kila kitu.Hisia miongoni mwa wananchi zimegawanyika. Nusu ya wananchi bado wanamwona Merkel kuwa ni kiongozi mzuri. Lakini wengin...

Waziri wa Fedha alia na Wafanyabiashara wadanganyifu.

Waziri wa Fedha alia na wafanyabiashara wadanganyifu http://www.mwananchi.co.tz/habari/biashara/Waziri-wa-Fedha-alia-na-wafanyabiashara-wadanganyifu/1597570-3361464-12n89t4z/index.html

Vichwa vya Habali katika Magazeti ya leo Jumatatu August 29, 2016

Picha
Nime kukusanyia Yote ya Leo pata vichwa vya habali vya Magaezi August 29, 2016.

Godbless Lema Agoma Kula kwa Saa 48

Godbless Lema Agoma Kula Kwa Saa 48 http://www.mpekuzihuru.com/2016/08/godbless-lema-agoma-kula-kwa-saa-48.html?m=1

William Lukuvi;Serikali imeanza kupima Ardhi

Picha
Waziri wa Aridhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amesema kuwa Serikali imeanza kazi ya kupima ardhi  nchi nzima kuanzia mkoani Morogoro. Akizungumza  katika kipindi kipya cha "TUNATEKELEZA" kinachoandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO na TBC1 ,alisema utekelezaji wa zoezi hilo umeanzia mkoani humo ili kupima maeneo ya wakulima na wafugaji na kutatua migogoro ya ardhi Mkoani humo. “Serikali tumedhamiria kumaliza migogoro ya ardhi, kutimiza ndoto ya Rais Magufuli ya kuondokana na migogoro ya ardhi isiyo na tija inayosababisha watu kupoteza maisha’’Alisema Lukuvi  Ameongeza kuwa katika upimaji huo wa ardhi serikali inashirikiana na kampuni binafsi zilizosajiliwa ili kumuwezesha mwananchi anayemiliki shamba,kiwanda ,mkulima na mfugaji mwenye eneo  kupimiwa na kuongezewa thamani.  “Nakuhakikishia katika kipindi cha miaka 10 kila kipande cha ardhi Tanzania kitakuwa kimepangwa na kupimwa utaratibu mzuri utakao mwezesha kil...

Walimu Waonekana,Sasa waingia Kwenye Ajira.

Picha
KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa imeomba Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa imuombe Rais atoe kibali cha ajira kwa walimu kukabili uhaba unaoikabili nchi. Mwenyekiti wa kamati hiyo, Jasson Rweikiza alitoa ushauri huo jana mjini Dodoma kwenye kikao kati ya wajumbe wa kamati hiyo na viongozi na watendaji wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa wakiongozwa na Naibu Waziri, Selemani Jafo. Kikao hicho kilikuwa ni cha kamati kupokea na kujadili taarifa ya tathmini ya utekelezaji wa mpango wa ofisi hiyo wa utoaji elimu bila malipo katika kipindi cha Januari hadi Juni mwaka huu ambako suala la uhaba wa walimu liliibuliwa na wajumbe. “Walimu waajiriwe...ni vyema mumuone rais, angalau afungulie kibali cha walimu pekee...wanafunzi wanaongezeka mara mbili, lakini walimu hakuna,” alisema Rweikiza. Awali, akijibu hoja za wajumbe juu ya changamoto ya uhaba wa walimu, hususan wa Sayansi na Hisabati, Jafo alikir...

Askari wa Jesh la Mgereza kuingia Hospital na Bunduki

Picha
  Askari wa Jeshi la Magereza mkoani hapa amezua taharuki kwa wagonjwa baada ya kuingia hospitalini na bunduki na baadaye kufyatua risasi kadhaa hewani. Tukio hilo lilitokea wakati usalama wa askari na silaha zao, ukizidi kuwekwa kwenye hali ngumu baada ya kutokea matukio kadhaa ya polisi kuvamiwa, kuuawa na kuporwa silaha na watu wasiofahamika kudiriki kuvamia hata vituo vya polisi na kupora silaha. Juzi usiku saa 4.00, askari jela huyo aliingia hospitali kumuangalia mwanaye aliyelazwa akihudumiwa na mkewe. Mganga Mkuu wa Mkoa, Dk John Gurisha alisema askari huyo aliingia wodi namba 10 ambako mke wake alikuwa amelazwa na mtoto. Kamanda wa Polisi Mkoa, George Kyando amesema chanzo cha askari huyo kufanya hivyo ni ulevi uliopindukia. Amesema mtuhumiwa anaendele kuhojiwa na atafikishwa makamani wakati wowote. “Tunaendelea kuchunguza ili baada ya uchunguzi kukamilika, sheria ichukue mkondo wake,” amwsema Kyando.