Tanapa Kuongeza Watalii Hifadhi ya Taifa ya Ruaha.
WETUIMECHAPISHWA: 31 AGOSTI 2016
Meneja Mawasiliano wa TANAPA, Pascal Shelutete akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) wilayani Mbarali namna ambavyo TANAPA ilivyojipanga kwa ajili ya tukio la kupatwa kwa jua litalotarajiwa Septemba Mosi. Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Mbarali, Reuben Fune.(Mpigapicha Wetu)
SHIRIKA la Hifadhi za Taifa (TANAPA) limetangaza kutumia tukio la kupatwa kwa jua linalotarajia Septemba mosi mwaka huu kufungua lango la Ikoga katika wilaya ya Mbarari mkoani Mbeya ili kuongeza watalii katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha.
Kufuguliwa kwa lango hilo kunafanya idadi ya milango ya kuingia katika hifadhi hiyo kufikia miwili ukiacha lango kuu la Way Junction ambalo limekuwa likitumika kwa muda mrefu sasa.
Meneja Uhusiano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete anasema kuongezeka kwa lango la Ikoga ni fursa kubwa ya kuhamasisha utalii wa ndani kwa kuwa eneo la Ihefu lina kivutio kikubwa cha wanyama wa aina mbalimbali.
Mkuu wa Wilaya ya Mbarali, Reuben Mfune, anasema Wilaya hiyo ina vivutio vingi, hivyo amewataka wananchi watakaofika kuangalia kupatwa kwa jua, kutumia fursa hiyo kutembelea vivutio vilivyopo Wilayani humo.
Tukio la kupatwa kwa jua linatarajiwa kutokea Septemba mosi majira ya saa nne asubuhi hadi saa nane mchana katika kata ya Rujewa eneo la Mpunga Relini Kiometa 3.5 kutoka barabara kuu ya kutoka Dar es Salaam-Mbeya.
Maoni