Simba Kumpeleka Kessy Mahakamani.

Simba imepanga kumpeleka Kessy mahakamani kwa madai ya kuwatuhumu viongozi wa Simba kuwa walitaka kumpa rushwa

Klabu ya Simba imejiridhisha na kupeleka ushahidi kwenye kamati ya sheria na hadhi za wachezaji kuhusu sakata la usajili linalomhusu beki wa kulia wa Yanga Hassan Kessy Ramadhani na wanaamini endapo haki itasimamiwa vilivyo basi watashinda kesi hiyo.

“Yanga walituandikia barua, TFF wakiomba kupewa leseni ya mchezaji Kessy kabla ya June 15 ambapo ndio ulikuwa mwisho wa mkataba wake, tena walikuwa wanamuombea leseni ya CAF lakini kimantiki huwezi kupewa laseni ya CAF bila kuwa na leseni ya ndani”, amesema Haji Manara afisa habari wa Simba wakati akizungumza na waandishi wa habari.

“Kwahiyo kimsingi, Kessy alivunja mkataba, Yanga walimchezesha mchezaji ambaye aliwekewa pingamizi.”

Wakati huohuo klabu ya Simba imepanga kumpeleka Kessy mahakamani kwa madai ya kuwatuhumu baadhi ya viongozi wa Simba kutaka kumpa rushwa wakati akiwa Mtibwa Sugar.

“Hatutaki kuombwa radhi kwasababu katutuhumu kila mtu kasikia nchi nzima, lazima akathibitishwa mahakamani. Lakini akanithibitishie mimi niliwahi kumwambia yeye atachoma banda”, alimalizia Manara.

Maoni

Hot News alisema…
sahii
kabisa

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Miamala ya Benk na Simu,Imezaa matunda.

Matangazo ya vyakula mitandaoni huponza watoto