TANZANIA YETU.
MAONO YA MWONAMBALI.
Nchini Tanzania haswa upende wa Serikali za Mitaa,tunatambua kila baada ya miaka 5 kunachaguzi zinafanyika.Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambapo tunachagua Wenyeviti wa Vitongoji,Wenyeviti wa vijiji/mitaa na uchaguzi Mkuu wa Madiwani,Wabunge pamoja na Uchaguzi wa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Katika chaguzi hizi ,wote Hawa uchaguliwa na Wananchi katika maeneo yao.
Mwenyekiti wa Kitongoji-Ambaye anachaguliwa na Wananchi wa Kitongoji husika.
Mwenyekiti wa Kijiji/Mtaa -atachaguliwa na Wananchi wake kupitia chama alichopendekezwa.
Madiwani -Uchaguliwa na Wananchi katika kata husika kupitia chama alichopendekezwa.
Wabunge -Pia uchaguliwa na Wananchi katika Jimbo husika.
Raisi-Atachaguliwa na Wananchi ndani ya nchi.
Katika makundi yote hayo matano ambayo wanapewa dhamana na Wananchi.Timu ya wenyeviti wa vijiji , Vitongoji na Mitaa wamesahaurika kwa namna ifuatayo:-.
1-Madiwani wanaposho na wakimaliza muda wao wa kutumikia wananchi wanalipwa chochote Kitu.Mwenyekiti wa Kitongoji wa Mtaa na wakijiji hakumbukwu kwa chochote.
2-Wabunge wanaposho na wakimaliza muda wao wa kutumikia wananchi wanalipwa chochote Kitu.
3-Raisi-(..........)
Tukumbuke wote wanachaguliwa na Wananchi.
Ombi langu Serikali iwaangalie Wenyeviti wa Vitongoji,Kijiji na Mtaa ili kuongeza ufanisi wa kusimamia shughuli mbalimbali za maendeleo ya Nchi yetu katika maeneo yao ya Kazi.Kwani wanafanya kazi Kubwa katika kuwatumikia wananchi wa nchii.
Imeandikwa na ;-
............
Kwa pamoja tunaweza.
Maoni